Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) pamoja na AB InBev na WWF Africa wameandaa Warsha ya Maji jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 25–27 Oktoba 2022.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa WWF Tanzania Amani Ngusaro amesema “Hali ya maji kwa sasa si nzuri kwani mito mingi imekauka hadi kupelekea wanyama maeneo mengi sana kuathirika.
Hivyo ushirikiano huo kati kampuni ya TBL – AB InBeV, pamoja na WWF unasukumwa na nia ya pamoja ya kuboresha ubora na wingi wa maji katika maeneo yaliyoainishwa yenye hatari kubwa ifikapo 2025.
Semina ya mwaka huu 2022 imebeba mada ya, “Usalama wa Maji kwa ajili ya Afrika”, ni fursa kwa wanamasoko wa WWF pamoja na AB InBev, wadau kutoka Serikalini, na washirka mbalimbali kubadilishana ujuzi na maarifa, kupeana miongozo thabiti, na kuendesha swala la usalama wa maji katika jamii zetu.
Pia amesema WWF peke yake haitaweza kwenye janga hili la maji bali hata kampuni nyingine za vinywaji vingine na taasisi zingine ambazo hazihusiki na maji na ambazo zinahusika na maji kwa pamoja ziungane wamuunge mkono Mh Rais Samia kupigana na vita hii.