Top Stories

Hamad Rashid Mohamed kuhusu kesi yake na CUF Mahakamani, kufukuzwa, kuuawa.. Kuchokwa? (Audio)

on

DSC09967

Hamad Rashid Mohamed alikuwa Mjumbe wa Baraza Kuu CUF, lakini baadae alifutwa uanachama January 4 2012 na Baraza la Uongozi la chama hicho kutokana na madai kuwa alikuwa akikihujumu Chama hicho.

DSC09965

Baadae 2014 akaibuka tena na kutangaza Kugombea Urais wa Zanzibar kwenye Uchaguzi Mkuu 2015, July 23 2015 kimefanyika Kikao cha Chama cha ADC kwenye Hoteli ya Peacock Hotel  Dar es Salaam, ambapo Hamad Rashid amekabidhiwa Kadi ya Chama hicho.

Mwaka 1977 nikigombea Ubunge wa KUSINI PEMBA niliambiwa kwenye Siasa kuna mambo matatu mara nyingi wanasiasa na wanadamu yanawakuta, kufukuzwa, kuwekwa ndani na kuuawa… nikasema bora nisiende kwenye Siasa lakini nikaambiwa yatakukuta hata nje ya Siasa, hata viongozi wa Dini na Manabii yamewakuta.. Nikaambiwa jambo kubwa la kufanya ni kumtanguliza Mwenyezi MUNGU kwa kila jambo” >>>> Hamad Rashid Mohamed.

DSCI0160

Hamad Rashid alipokabidhiwa kadi yake.

Nawashukuru Watanzania na Wazanzibari wamekuwa pamoja na mimi katika misukosuko ya Siasa iliyonikuta mpaka leo ADC mmenipokea… Wakati nawashauri ADC kwamba kama mnataka kuanzisha Chama jambo la kwanza tambueni uwepo wa Mwenyezi MUNGU… mtapambana na Rushwa, Ufisadi na kila dhuluma kwa sababu mmemuweka MUNGU mbele” >>>>

Hapa akaongelea ishu ya kesi yake na Chama cha CUF ambayo ilikuwa Mahakamani >>>> “Jana tulikuwa tumemaliza kesi na CUF, tulipoenda Mahakamani Jaji nikaambiwa hayupo lakini msajili wa Mahakama yupo… akasema yeye anaweza kuliondoa shauri lakini hawezi kuondoa gharama za kesi.. nikamwambia naenda Kugombea Urais nikimsubiri Jaji mpaka September wataniwekea pingamizi nisiingie kwenye Uchaguzi.. cha msingi kesi imeisha na niko tayari kupokea kadi ya ADC, waliokuwa na mashaka na hilo nimemaliza” >>>> Hamad Rashid Mohamed.

DSCI0184

>>>> ‘Nimefukuzwa CCM na nimefukuzwa CUF, mimi sijawahi kutoka katika Chama.. mimi sio malaya wa Kisiasa hata kidogo… Msimkasirikie mtu anayetaka kuhamia Chama kingine, ni uhuru wake na haki yake… Waliokuwa na mashaka wanauliza unakwenda ADC au ACT, niko ADC… ACT ni nyingine na ADC ni nyingine, wasiwe na mashaka kuna Uongozi uliokomaa” >>> Hamad Rashid Mohamed.

DSCI0167

Hapa iko sauti yake yote, bonyeza play umsikie Hamad Rashid Mohamed.

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments