Stori Kubwa

Maneno ya James Mbatia alivyomkaribisha Edward Lowassa UKAWA… (Audio)

on

imageHeadlines baada ya headlines kuhusu siasa Tanzania zina uzito mpya kila siku… Imeandikwa sana Magazetini kuhusu Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa kuhama CCM, kilichoteka headlines July 27 2015 kimeongezea uzito kwenye ishu hiyo.

Viongozi wa Vyama vya UKAWA, Emmanuel Makaidi, Prof. Lipumba, Freeman Mbowe na James Mbatia wamekutana Makao Makuu ya CUF Buguruni Dar na kutoa majibu kuhusu kumpokea Edward Lowassa.

Uchaguzi wa October 2015 ni fursa ya kipekee ya kuleta mabadiliko katika nchi yetu kuondoa ukandamizi uliojikita CCM… Watanzania wanahitaji Mabadiliko yenye fikra mpya na bunifu kwa maslahi ya Watanzania wote“>>> James Mbatia.

UKAWA tunahitaji Viongozi wenye sifa, uwezo na weledi katika kulinda, kuheshimu na kusimamia rasilimali za Taifa kwa maslahi ya Taifa.. Nachukua fursa hii kumualika Mheshimiwa Lowassa ajiunge na UKAWA na tuko tayari kushirikiana nae kuiondoa CCM madarakani” >>>> James Mbatia.

Bado Mbunge Edward Lowassa hajajibu chochote kuhusu kuendelea na CCM au kuhama, maneno ya James Mbatia yako hapa kwenye hii sauti.

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments