Mix

Dereva hakushtuka mpaka hili basi likaja kunasa hapa chini ya daraja Ufaransa… (Picha)

on

Basi Ajali II

Kama kuna ajali ambazo zimewahi kunishtua ni hii hapa, kwanza najiuliza dereva hakuona au ilikuwaje mpaka hii basi ikanasa hapa!

Ndani ya Basi kulikuwa na Wanafunzi 60 wa Kihispania, wametoka zao Bilbao kwenda Amsterdam bahati mbaya hii ajali ikatokea wakiwa eneo la La Madeleine, Ufaransa… Mwanafunzi mmoja amesema wengi wao walikuwa wamelala ndani ya basi, wakashtukia tu gari imenasa chini ya daraja na imekatika sehemu yote ya juu.

Majeruhi wengi walikuwa waliokaa kwenye siti ya nyuma, walipelekwa Hospitali na wengine ilibidi waahirishe tour yao na kurudi nyumbani kwao Hispania.

Basi Ajali

Dereva alikamatwa na kupimwa wakakuta hakuwa amelewa wala hakuwa na tatizo lolote, alichojitetea ni kwamba alikuwa akifata maelekezo ya barabara kwa kutumia GPS na hakuwa amegundua kwamba daraja hilo lina urefu ambao basi lake haliwezi kupita !!

Hii video ni ajali ya aina hiyohiyo iliyotokea Uingereza 2013, basi likakatika baada ya kupita chini ya daraja la treni.

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments