Michezo

Serengeti Boys wameianza safari ya kuibakiza AFCON U-17 nyumbani

on

Timu ya Taifa ya Vijana U17 “Serengeti Boys na Timu ya Taifa ya Vijana U20 “Ngorongoro Heroes” zimeondoka kuelekea Rwanda na Eritrea.
.
Serengeti Boys wapo nchini Rwanda na Kikosi cha Wachezaji 23 na viongozi 8 kushiriki mashindano maalumu ya maandalizi ya AFCON ya Vijana U17 itakayofanyika Tanzania April 14-28,2019.
.
Mashindano hayo maalumu ya Kimataifa yatajumuisha timu 3, Serengeti Boys, Cameroon na wenyeji Rwanda ambapo kila mmoja atacheza na mwenzake, yanatarajia kuanza Machi 28-Aprili 4,2019 Kigali,Rwanda.
.
Kikosi cha Ngorongoro Heroes wenyewe wapo Asmara Eritrea watakapocheza mchezo wa Kirafiki na Eritrea Machi 31,2019 nchini humo, jumla ya Wacheza 20 na Viongozi 8 wapo katika msafara huo.
.
Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars

Soma na hizi

Tupia Comments