Top Stories

Kutoka kwenye Mkutano wa CCM Dar July 29 2015>>> Dk. Magufuli, Uchaguzi 2015.. Lowassa kuhama? Wengine waliotoka?

on

3X6A9995

Kulikuwa na tangazo ambalo lilienea sana mitandaoni kuanzia July 28 2015 ikiwa na taarifa kwamba CCM watafanya Kikao chao Makao Makuu Madogo July 29 2015 Lumumba Dar.

CCM Dar

Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Dar, Juma Simba Gaddafi ndio Kiongozi pekee wa CCM aliyefika kwenye Mkutano huo ambao umefanyika Peacock Hotel Dar, na hii ni sehemu ya alichokisema.

CCM inatoa shukrani kwa ushirikiano mlioutoa katika Mkutano wetu Mkuu wa Kumtambulisha Mgombea Urais Dk. Magufuli pale Mbagala, CCM ni Chama chenye busara tumeona tuwashukuru‘>>>

3X6A9984

Kwenye sentensi nyingine amesema hivi >>> ‘Tume ya Uchaguzi tunawaomba wawe makini kuongeza Mashine na Watendaji ili watu wapate nafasi kujiandikisha na watumie fursa yao Kupiga Kura… CCM tuna uhakika tutashinda‘>>>

3X6A0023

Juma Simba Gaddafi, Katibu wa Siasa na Uenezi Dar CCM Dar.

Kingine tunawashukuru waliojitokeza Kugombea nafasi mbalimbali za Ubunge na wajitokeze kwa wingi pia kupiga kura… Tumemaliza Uchaguzi Dodoma na kumpata Mgombea wetu Dk. Magufuli, tunajivunia kwa sababu ana rekodi nzuri… Tuna imani CCM itaendelea kuongoza 2015 mpaka 2020, tumefanya mengi yanayokubalika‘>>>

3X6A0039

Hiki ndio alichokijibu kuhusu ishu ya Lowassa kuhamia CHADEMA >>> ‘Yeye aliingia CCM kwa ridhaa yake hakuna mtu alimlazimisha, ametoka kwa ridhaa yake na CCM itabaki kuwa CCM… Wafuasi walikuwa ndani ya CCM, kuondoka kwake ameondoka yeye na sio wa kwanza kuondoka‘>>>

3X6A0063

Haya ni majibu yake mengine kuhusu Lowassa kutoka CCM >>> ‘Mtu akitoka huwezi kujibu kwa nini ametoka, nawathibitishia mtu yoyote akitoka CCM itabaki imara… Tutashinda asubuhi kweupe… Kama Lowassa angekuwa anaondoka na watu wengi ungewaona jana, lakini alikwenda yeye akarudisha kadi… watu wengi wanatoka kwenye Chama na CCM bado iko imara‘ >>>> Juma Simba Gaddafi.

Hiki ndio alichokijibu kuhusu Uteuzi wa Mgombea wa Urais CCM Dodoma >>>>’Mkutano Dodoma tuliumaliza, lakini tumekwenda kwenye NEC Wajumbe wako 360, walipiga kura majina matano na Wagombea wote wa Halmashauri Kuu akiwepo Rais, Waziri Mkuu na Lowassa walikuwepo… kama asingekuwepo hayo yangesemwa, lakini alishiriki na alipiga Kura‘>>>>

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments