AyoTV

Nakupeleka mpaka Durban South Africa kukutana na jengo kulikotolewa tuzo za MTV Africa 2015

on

MTVInawezekana sababu mojawapo ya utolewaji wa tuzo kubwa za burudani Afrika kufululiza kufanyika Afrika Kusini ni kutokana na urahisi wa sehemu ya kufanyikia yani majengo sahihi kwa ajili ya events kubwa kama hizi ambapo MTV Mama Awards 2015 zilitolewa hapa July 18.

Durban Arena 2Ni nchi iliyoendelea sana Afrika kwa kuwa na miundombinu mizuri kama barabara na hata majengo ambayo yanaweza kutumika kwa matukio kama haya ya MTV Mama Awards ambapo event ilifanyika kwenye ukumbi wa ICC Durban South Africa.

Durban Arena 3Ni ukumbi ambao June 2015 uliendeleza headlines zake kwa kupigiwa kura kwenye tuzo ya kuwa ukumbi bora wa mikutano Afrika kwa mara ya kumi na nne mfululizo kutokana na ubora wake, ujenzi wa kisasa na hata urahisi wa kupata huduma muhimu unapokuwa ndani yake.

Durban Arena 4Kwa mara nyingine tena tuzo za MTV Africa 2015 zilifanyika ndani ya hili jengo ambapo Tanzania ilikua ikiwakilishwa na wawili ambao ni Diamond Platnumz aliyeshinda tuzo ya BEST LIVE pamoja na Vanessa Mdee.

Unaweza kutazama sehemu tu ya hili jengo na watu walivyojitokeza kwenye hii video hapa chini..

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments