Stori Pekee

Polisi kamsimamisha jamaa akamkuta na kosa akasema pesa ndio tatizo…. maamuzi haya ya Polisi yakafatia

on

Police 3Ni kawaida kwenye mataifa karibu yote duniani, unapokamatwa na Polisi ukakutwa na kosa ni aidha ulipie faini, akusamehe, ujirekebishe ulichofanya au wengine uwape hongo ya kuwapooza ili akuachie ukafanyie kazi ulichokosea ila hii ilitokea Marekani ni ya kipekee.

Jamaa alivyokamatwa na kukutwa na kosa la document yake kuisha muda wa matumizi huku akitakiwa kununua sticker nyingine, alimwambia Polisi kwamba amekua na tatizo la kuimudu pia familia yake ya mke na watoto wawili hivyo hiyo ndio sababu pekee imemfanya ashindwe kupata pesa ya kulipia hiyo document muhimu kwenye gari.

Baada ya hapo Polisi huyo akaingiwa na huruma akampa pesa ili akamalizane na hilo kosa, ambapo alimpa USD 100 ambayo kwa leo ni zaidi ya shilingi laki mbili za Kitanzania ambapo baada ya kutenda wema Askari huyo hakutaka jina lake litajwe wala sura yake ionyeshwe.

Unaweza kutazama hii video ya tukio lenyewe hapa chini alafu ukishamaliza uniambie kwenye comment ni kitu gani kizuri Askari amewahi kukufanyia?

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments