Duniani

Polisi wa Brazil walivyomkimbiza mtuhumiwa kwa Helikopta na kummiminia risasi kwa juu.

on

Brazil PoliceBrazil ipo kwenye list ya nchi ambazo huwa zina matukio makubwa ya mara kwa mara ya kihalifu, ukiachia mbali ishu za dawa za kulevya, kuna uhalifu mwingine ambao huwa unafanyika ikiwemo kwenye foleni barabarani kama hujafunga kioo cha gari kuna wezi wanakuja na pikipiki wanakuonyesha bastola ili utoe kila kitu.

Tukio lilitokea June 2015 ambapo wanasema hii video hapa chini imetolewa makusudi kama fundisho kuonyesha ni jinsi gani unaweza kujikuta matatizoni pale unapowakimbia Polisi, ni bora kujisalimisha na mkamalizana kwa utaratibu kuliko kurushiwa risasi ukiwa ndani ya gari lako kama inavyoonekana kwenye hii video ambapo mtuhumiwa alirushiwa risasi ikampata mguuni akiwa ndani ya gari alilolisimamisha baada ya kuanza kuyumba.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments