Stori Pekee

Kwenye hii jeans unaiweka simu yako poa kabisa, inachaji huku unaendelea na mambo mengine (Pichaz)

on

a750cc907355c50ed59c150f3dc687524724a746

Kumegunduliwa powerbank ambazo zinaokoa sana watumiaji wa smartphone, lakini ubunifu haujaishia hapo… sasahivi zimekuja mpaka jeans, ndio…. Unavaa suruali yako fresh kabisa alafu unatundika na smartphone yako na betri yake inaendelea kuingiza chaji mdogomdogo!

Jeans yenyewe imeingizwa sokoni Marekani kwa dola 189 (Tshs. 400,000/= kwa sasa), utaweza kuchaji smartphone yako alafu kila kitu kinakuwa sawa… usihofu kwamba simu yako itaanguka, kuna sehemu poa ya kuweka simu pamoja na betri yenye chaji ili iendelee kuchaji simu yako popote ulipo.

Sehemu ya kuweka simu ni kama kimfuko hivi juu ya mfuko wa nyuma wa jeans, ila kama simu yako ni kubwa kuliko iPhone 6 basi itakuwa bahati mbaya yako, haitoweza kuingia.

charging-pants-phone-today-inline-150810_808432cd5778386d83785767af933f75.today-inline-large

joes-2-600x236

Hapo unaichomeka simu yako, na Powerbank au betri ili iendelee kuingiza chaji kwa urahisi zaidi bila kujiongezea mizigo mkononi… Jeans yenyewe inaitwa #Hello Jeans, ni ubunifu wa Joe’s Jeans.

ced3169d090039e8d190804d5107ded5103433ce

Unaweza kucheki kwenye hiki kipande cha video jeans hiyo ilivyotengenezwa.

https://www.youtube.com/watch?v=k-kOgjeiNuU

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments