Top Stories

Nape Nnauye kuhusu walioihama CCM, Mbowe kuuza CHADEMA, Lipumba na Dr. Slaa, Magufuli na Laptop (+Audio)

on

2

Kinachosubiriwa sasahivi Tanzania moja ya matukio makubwa sana mwaka 2015 ni ishu ya Uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani ambao utafanyika October 25 2015… Kuna ishu ambayo iliandikwa na baadhi ya Magazeti ya Tanzania na baadae ikagusa pia kwenye Mitandao ya Kijamii ilihusu ahadi ambayo ilidaiwa kutolewa na Mgombea Urais wa CCM, Dk. John Pombe Magufuli.

Nape Nnauye katoa majibu kuhusu ahadi hiyo leo >>> “Kuna kauli inayodaiwa kuwa ya John Magufuli inayodai kwamba atawanunulia Walimu kompyuta nchi nzima… Magufuli hajawahi kuzungumzia suala hilo popote, kuna watu wanajaribu kuitengenza na kujaribu kuonesha kuwa ameanza kampeni… muda wa kampeni bado, wakati huo ukifika tutayazungumza.. wanaojaribu kutengeneza habari za uongo waache” — Nape Nnauye.

4

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye.

Kwenye sentensi nyingine Nape Nnauye ameyasema haya >>>> “Hivi kweli mtu ambaye amejiandaa leo sio tu Prof. Lipumba hata Dk. Slaa wamejiandaa muda mrefu sana na wakapewa matumaini na chama chao halafu dakika ya mwisho anatoka jamaa anakinunua chama… Freeman ameuza CHADEMA amemuuzia Lowassa” >>>> Nape Nnauye.

1

Hiki ndio alichokijibu kuhusu wanaohama CCM >>> “Hakuna kiongozi wa upinzani ambaye ameanzisha upinzani hakuanzia CCM, hata hao wanaoondoka.. waliondoka na watakaoondoka wanafata mkumbo uleule wa wenzao… wengi wao wanaondoka kwa sababu ya matatizo yao binafsi” >>> Nape Nnauye.

Sauti ya Nape Nnauye iko hapa pia mtu wangu, unaweza kubonyeza pplay kusikiliza kila kitu kutoka kwake.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments