Duniani

Hii ndio Kampuni iliyovunja Rekodi kununua ndege 250 kwa wakati mmoja.. !! (+Video)

on

Indigo

Hii imeingia kwenye rekodi kubwa za duniani 2015, inahusu ishu ya Kampuni moja ya Ndege kusaini dili ya kununua ndege 250 kwa wakati mmoja, tena ni ndege kubwa za abiria !!

Kampuni kubwa ya kutengeneza Ndege Duniani ya Airbus imesaini hiyo dili ya kuwauzia Kampuni ya IndiGo ya India ndege hizo 250 aina ya Airbus A320neo.

Hii sio mara ya kwanza IndiGo kununua Ndege nyingi kwa wakati mmoja, mwaka 2005 IndiGo Airlines ilinunua jumla ya ndege 100 kutoka Kampuni hiyo hiyo ya Airbus… biashara yao mpya ni hii ya kuuziana ndege 250 ambapo ndege hizo zitagharimu kama Dola Bilioni 26.5 (Zaidi ya Trilioni 54 kwa Tshs sasahivi).

IndiGo Airlines ilianzishwa mwaka 2006 na ni moja ya Makampuni makubwa sana India inayomilikiwa na Mabosi wawili, Rahul Bhatia na Rakesh Gangwal.

India II

American Airlines nao waliwahi kuandika Rekodi yao kubwa mwaka 2011 kwa kuagiza ndege 460 kwa wakati mmoja, lakini kwa 2015 IndiGo Airlines pekeyao ndio waliogonga hiyo rekodi kubwa kununua Ndege nyingi zaidi kutoka Kampuni ya Airbus !!

Stori iko kwenye hii video pia

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments