Mix

Matusi mitandaoni Tanzania mwisho ilikua jana saa tano na dk 59 usiku ! fahamu mengine ya sheria mpya hapa

on

Huu ndio utakua mwisho wa makosa ya kimtandao Tanzania??? sababu sheria hii imepitishwa na kuanza kutumika leo mahususi kwa wote wanaotumia vibaya mtandao.

Unaambiwa mwisho wa yote ulikua jana August 31 2015 sababu leo September 1 2015 sheria hii ndio imeanza kutumika rasmi baada ya kupitishwa na Bunge mapema 2015 na kusainiwa na Rais Kikwete ikiwa ni miongoni mwa sheria zilizopitishwa na bunge kwa hati ya dharura.

Unafahamu sehemu ya makosa ambayo yanaweza kukufanya ushtakiwe?

  • Kuweka mtandaoni picha za kingono za watoto
  • Kuweka mtandaoni picha za ngono au za utupu
  • Kuweka taarifa za uongo mtandaoni
  • Kuweka taarifa za uchochezi mtandaoni
  • Kutukana au kumdhalilisha mtu
  • Kuweka mtandaoni tetesi zisizothibitishwa
  • Kutukana au kumdhalilisha mtu kwa misingi ya udini/ukabila.

Innocent Mungi kutoka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) anasema >>>Ambaye atakua anachukua maamuzi ni jeshi la Polisi ambaye kwa mfano mtu akitukana kwenye mtandao au kufanya chochote kinyume na sheria yule aliyetendewa anao wajibu wa kulalamika kwa Polisi, watafanya uchunguzi alafu mwendesha mashtaka ataifikisha hiyo kesi kwa Jaji ambaye ndio atafanya maamuzi kutokana na kesi yenyewe

Sisi kama TCRA tunaweza kuitwa kama mashahidi kwenye hizo kesi, kwahiyo kuanzia August 31 2015 yale maswala ya mazoea ya NATUMA KAMA NILIVYOPOKEA au NINALETA KAMA NILIVYOIOKOTA HUKO, jihadhari sana kwa mfano yule aliyetengeneza amempelekea mtu mmoja lakini wewe umesambaza kwenye group lako la Whatsapp mko 100, utashtakiwa‘ – Innocent Mungi

BONYEZA PLAY KUMSIKILIZA INNOCENT MUNGI HAPA CHINI

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments