Habari za Mastaa

Mwaka 2015 nimepata pesa nyingi kwenye muziki kuliko miaka mingine – Mr Blue

on

Jina lake ni Herry Samir lakini kwenye muziki tunamuita Mr Blue. Mwaka 2015 huyu jamaa hawezi kuusahau kutokana na kuwa na vitu muhimu kwenye maisha yake.

Kikubwa na cha kwanza ni kupata mtoto wa kike ambae ameongeza idadi ya familia ya Mr Blue kutoka kuwa watu watatu hadi wanne. Hivi sasa Mr Blue ana watoto wawili wa kike na wakiume.

Sasa Mr Blue amesema kwamba mwaka 2015 ndio mwaka ambao amefanikiwa kutengeneza pesa nyingi sana kuliko miaka yote kwenye maisha yake ya muziki. Japokua hajataja kiasi alichoingiza lakini Mr Blue anasema kutokana na kazi zake za show kwa mwaka huu ndizo zimefanya kuvunja rekodi ya miaka yote iliyopita.

Vyanzo vya pesa hizo ni kutokana na show, mauzo ya nyimbo mtandaoni, caller tune na vitu vinavyohusiana na muziki.

Mr Blue alimaliza mwaka jana kwa kufanya show kali ya Fiesta Dar es salaam na mikoani kitu ambacho kilionyesha bado kuna mashabiki wengi wanamkubali na ku-miss show zake.

bbb

Watoto wa Mr Blue

Tupia Comments