Mix

Video: Waziri mkuu wa Hispania alivyopigwa ngumi katikati ya kampeni, tukio la pili ndani ya wiki

on

Siku zinahesabika toka Waziri mkuu wa Ukraine alipobebwa juujuu akiwa bungeni, aliyembeba alijifanya kama anampelekea ua alafu baada ya kufika akambeba juujuu kabla hajashambuliwa kwa kipigo na baadhi ya waliokuwemo bungeni, sasa December 16 2015 habari ya zamu ya Waziri mkuu wa Hispania.

Waziri mkuu wa Hispania Mariano Rajoy alipigwa ngumi usoni na kijana ambaye alikua pembeni yake wakati akiongea na wapiga kura kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa Hispania.

Waziri mkuu huyu kutoka chama ambacho kinatajwa kuwa na asilimia kubwa ya kuibuka mshindi pamoja na kwamba kimelalamikiwa kwa rekodi ya vijana kukosa ajira kuongezeka, alipoteza miwani yake lakini imeripotiwa na gazeti la Hispania kwamba alipata tu alama nyekundu usoni kwake.

Spain 2

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments