Michezo

Tabasamu la Ronaldo kwenye headlines za mradi wa zaidi ya Bilioni 170 za kibongo …

on

Najua mwaka 2015 umekuwa wa headlines nyingi kwa staa wa soka wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo ambaye amerudi tena katika headlines na stori hii, Ronaldo ambaye kwa mwaka 2015 pekee amefanikiwa kuzindua perfume, movie ya maisha yake halisi na viatu, December 17 ameweka wazi project yake mpya.

2F77C9F200000578-3364672-image-a-1_1450379543965

Cristiano Ronaldo katika picha ya pamoja na partner wake Dionisio Pestana

Mshambuliaji huyo ambaye amekuwa akihusishwa kuihama Real Madrid mwishoni mwa msimu, ameingia katika headlines baada ya kuweka wazi project yake mpya ya kufungua hoteli, Ronaldo ametenga pound milioni 54 kwa ajili ya mradi wa kuanzisha hoteli katika miji ya Funchal, Lisbon, New York na Madrid.

2F77D0FE00000578-3364672-image-a-4_1450379637006

Ronaldo akiwa na wakala wake Jorges Mendes katika hoteli ya Pestana Palace iliyopo Lisbon kujadili idea ya mradi huo

“Kazi yangu ni kucheza mpira lakini maisha siku zote hayawezi kuendelea kuwa kama hivi, nimeamua kuingia mwenyewe katika mradi huu. mimi bado kijana na najihisi nimetimiza vitu vingi, hivyo nimeamua kuingia katika mradi huu, nafikiria kuhusu kesho yangu, mwanangu na familia yangu” >>> Ronaldo

2F77DEA200000578-3364672-image-a-3_1450379630494

Ronaldo akiingia ukumbuni kushoto ni nembo yake ya biashara ya CR7 na nembo ya biashara ya partner wake PESTANA

Cristiano Ronaldo anatajwa kuingia katika mpango huo kwa kushirikiana na Partner wa kireno ambaye anamiliki kampuni ya  Pestana Hotel Group. Ronaldo anatajwa kuwekeza pound milioni 54 ambazo ni zaidi ya bilioni 170 za kibongo, mkwanja ambao una thamani ya kujenga viwanja vitatu vya soka kama uwanja wa Taifa na chenji inabaki.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments