Habari za Mastaa

Lulu hakurudi Tanzania jana… ninacho alichoandika leo kuhusu kurudi kwake nyumbani na Tuzo

on

Tunajua ni Watanzania wawili walishinda tuzo mbili kwenye usiku wa tuzo za Africa Magic Viewer’s Choice Awards, wa kwanza ni Single Mtambalike ‘Richie’ na Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambapo Richie tayari alisharudi nyumbani Tanzania usiku wa March 6 2016 ila Lulu hakutokea Airport japo baadhi ya watu walimtarajia.

Lulu alishindwa kutokea jana akiambatana na Richie na kuiambia millardayo.com kwamba hakuweza kurudi hiyo jana sababu alibaki Nigeria kwa ajili ya kazi, kuna watu alikua na maongezi nayo kwenye nchi hiyo maarufu kwa filamu Afrika.

March 7 2016 Lulu amewajulisha Watanzania kwamba anarudi nyumbani siku ya March 8 2016 na atatua uwanja wa ndege Dar es salaam na akayaandika hayaTukijaaliwa uzima…kesho saa 8:30 (saa nane na nusu Mchana) nitaingia uwanja wa ndege Dar Es Salaam na mzigo wenu?au acha niseme Tuzo Yenu..!!???Can’t wait to see y’all?
(I’m hungry and I’m ready 4 change….TODAY?)

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE 

Soma na hizi

Tupia Comments