Michezo

Kutoka Mkwakwani Tanga Coastal vs Yanga mechi imeshindwa kumalizika

on

April 24 2016 ndio siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka Tanzania, kwani ndio ile siku ambayo ilikuwa inasubiriwa na mashabiki kushuhudia nusu fainali ya Kombe la FA (Azam Sports Federation Cup), kwa upande wa Yanga walikuwa wageni wa Coastal Union katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Kutoka katika uwanja wa Mkwakwani Tanga mechi imeshindwa kumalizika baada ya mashabiki wa Coastal Union kutoridhishwa na uchezeshaji wa refa hivyo mchezo umeshindwa kuendelea kutokana na kuwa na giza na vurugu za mashabiki, dakika 90 za mchezo huo ulimalizika kwa sare ya goli 1-1, hivyo muamuzi akaongeza dakika 30

qw

Bado haijajulikana maamuzi yatakuwaje kutokana na mchezo kuvunjika kutokana na uwanja kuwa giza lakini na hali ya usalama kuwa tete mashabiki wa Coastal walikuwa wanafanya fujo

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

ALL GOALS: Yanga vs Al Ahly (Full Time 1-1) April 9 2016 CAF

Soma na hizi

Tupia Comments