Top Stories

“Jamani huu Mjadala wa nguo fupi… haiwezekani Watu watembee na futi mitaani” – Tibaijuka

on

Kumekua na mjadala kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii baada ya habari kusambaa kwamba Wanawake wanaovaa nguo fupi na Wanaume wanaovaa milegezo, kunyoa viduku na suruali zilizobana Arusha na Dar es salaam wanakamatwa na Polisi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa alikanusha kuhusu Polisi Dar kukamata wanaofanya hivyo kwa kusema alinukuliwa vibaya.

Sasa baada ya kuona mijadala inaendelea kwenye mitandao ya kijamii, Mbunge wa Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka amejitokeza na kuongea yafuatayo >>> “Yani kuna vitu vingine huwezi kusema Muafrika alikua anavaa nguo ndefu, hapana sio kweli…”

Mwili wa Mwanamke unaonekana ni kifaa ambacho Mungu amekiweka kwa shughuli maalum ya Uzazi, Ulezi n.k sasa ambae anajiheshimu anajua nini cha kuvaa katika wakati gani, cha msingi ni maadili ya mavazi na pale ulipo

Hiki sio kitu ambacho kitasimamiwa huwezi tena kuwa tena na Watu wanatembea na futi mitaani kupima urefu au ufupi wa nguo, jamanijamani tunazo kazi nyingi za kufanya” – Profesa Tibaijuka …… msikilize zaidi hapa chini

MILLARD AYO NA WASHINDI WA MILIONI 10 ZA TATU MZUKA…. BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments