Mix

Kwa mara ya kwanza jiji la London limeweka historia mpya ya Meya ambaye sio mzawa

on

Alfajiri ya May 7 nchi ya Uingereza kupitia jiji lake la London imeingia kwenye historia mpya kwa mara ya kwanza, baada ya kupata meya wa kwanza muislamu na asiye na asili ya Uingereza Sadiq Khan, Khan ametangazwa rasmi. kuwa mshindi wa umeya wa London.

_89624265_khan2

Sadiq Khan

Khan ambaye alikuwa anagombea nafasi hiyo na wapinzani zaidi ya wawili, amefanikiwa kushinda umeya kwa asilimia 56.8 akifuatiwa kwa karibu na mshindani wake mkuu Tory Zac Goldsmith ambaye amefanikiwa kupata asilimia 43.2.

mayor

Baada ya kushinda Khan ambaye ana asili ya Pakistan kwa baba na mama ambao walihamia Uingereza miaka kadhaa iliyopita, alitoa kauli ya kwanza baada ya kutajwa mshindi wa umeya kwa kusemaMtu kama mimi kuchaguliwa kuwa meya wa London !!! sikuwahi kufikiria kwa kweli naahidi nitakuwa meya wa watu wote wa London

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments