Michezo

Simba imetangaza kumfungia mchezaji wake kwa kukosa uungwana na kuoneshwa kadi nyekundu

on

Baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba April 20 2016 kupitia kwa kocha mkuu Jackson Mayanja, afisa habari wake Haji Manara, nahodha wa timu Musa Mgosi pamoja na meneja wa timu Abasi wamejitokeza na kuongea na waandishi wa habari.

Viongozi hao wa Simba wamejitokeza na kuomba radhi mashabiki wa Simba ambao awali baada ya mchezo dhidi ya Toto Africans kumalizika kwa kufungwa goli 1-0 walimfuata Makamu wa Rais wa Simba Geofrey Kaburu na mwenyekiti wa kamati ya Usajili Zacharia Hans poppe na kuwatolea maneno yasio ya kiungwana pamoja na kutishia kuchoma basi la Simba.

DSC_1020

Kocha wa Simba Jackson Mayanja (kushoto) na Haji Manara wakati wa mkutano na waandishi wa habari

Pamoja na hayo Simba kupitia kwa afisa habari wake Haji Manara wametangaza kumuongezea adhabu beki wake wa kulia Hassan Kessy kutokana na kuoneshwa kadi nyekundu kwa kosa la kumchezea faulo mbaya Edward Christopher, kitendo ambacho kilimfanya muamuzi wa mechi amuoneshe kadi nyekundu ya moja kwa moja.

“Kessy juzi ameigharimu timu hatujui kwa makusudi au bahati mbaya, Kessy ameigharimu timu kwa kucheza rafu mbaya tena yenye nia mbaya kwa Edward Christopher kwa kumpandishia mguu kichwani kwa makusudi, licha ya kuoneshwa kadi nyekundu na refa na kukosa mechi mbili, Simba inamuongezea adhabu na kumfungia mechi 5” >>> Haji Manara

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

KAMA ULIIKOSA MECHI YA SIMBA VS TOTO AFRICANS  ILIYOMFANYA KESSY AFUNGIWE, FULL TIME 0-1.

Soma na hizi

Tupia Comments