Mix

Trending Worldwide: Mayweather kurudi ulingoni? Selfie inaweza kukusababishia kupoteza maisha

on

Huenda hukupata nafasi ya kusikiliza Amplifaya ya Clouds Fm Mei 2 2016 kutokana na kukosa time, lakini mtu wangu wa nguvu naomba nikuletee stori mbili zilizoingia kwenye headlines za Trending World Wide ya Amplifaya ya Clouds FM.

1- Bondia Floyd Mayweather   ambaye baada ya mchuano wake na Andre Berto September 17 2015  alitangaza kustaafu rasmi mchezo wa boxing, anaripotiwa kuwa kuna uwezekano wa kurudi kwenye mchezo huo.

Mayweather ambaye shindano lake na bondia kutoka  Filipino Manny Pacquiao lilitikisa dunia tarehe 2 May 2015 Las Vegas katika ukumbi wa MGM, bado hajaweka wazi kama atarejea ulingoni au hapana.

2- Mvulana wa miaka 15 Ramandeep Singh raia wa India  alijipiga risasi baada ya kujaribu kujipiga selfie na bastola ya baba yake …Ramandeep kwa sasa yupo hospitali na upo uwezekano wa kupona kama matibabu yakienda sawa.

Polisi  wanasema wanaweza kumlaumu baba wa  mvulana huyo kwa kuto kuhifadhi vizuri bastola hiyo ambayo ilikua na risasi. India imekua na matukio ya kufululiza ya aina hii ambapo tukio lingine lilimuhusisha mama mmoja ambaye alizama baharini wakati akijaribu kujipiga picha (selfie).

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

KAMA ULIMISS AGIZO LA KWANZA ALILOLITOA PAUL MAKONDA KAMA MKUU A MKOA ITAZAME HII VIDEO HAPA 

Soma na hizi

Tupia Comments