Mix

VideoFUPI: Watumishi hewa Kinondoni wamegundulika wapya, idadi yao ni zaidi ya asilimia 80 ya awali

on

Bado agizo la Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli la kuwatoa katika mfumo wa mishahara watumishi hewa linazidi kushika kasi kila kukicha, leo April 28 2016 mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi amethibisha kuongeza kwa idadi ya watumishi hewa.

Wilaya ya Kinondoni imebaini watumishi hewa wapya 55 baada ya uchunguzi wa awali kubaini watumishi hewa 34 pekee, sasa mkuu wa wilaya ya Kinondoni amethibisha rasmi kuwa wilaya ya Kinondoni imefikisha jumla ya watumishi hewa 89, watumishi hewa wa kwanza 34 walikuwa wanaitia serikali hasara ya zaidi ya milioni 500.

“Katika mambo ambayo mkuu wa mkoa aliniagiza niyafanyie kazi wakati nateuliwa na Rais ni watumishi hewa, nimekuta taarifa ya watumishi hewa 34 ambao walikuwa wameisababishia hasara serikali ya zaidi ya Tsh milioni 512, nilivyoteuliwa kuwa mkuu wa wilaya wiki moja iliyopita nimelifanyia kazi na kubaini watumishi hewa wapya 55” >>> Ally Hapi

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments