Michezo

Droo ya Kombe la Shirikisho Afrika imefanyika, Yanga kapangwa na klabu yenye miaka 39

on

Baada ya klabu ya Dar es Salaam Young Africans kuondolewa katika michuano ya klabu Bingwa barani Afrika usiku wa April 20 2016 na klabu ya Al Ahly ya Misri kwa jumla ya goli 2-1, sasa wanajiandaa kurudi kucheza Kombe la shirikisho barani Afrika katika hatua ya 16.

Yanga imepangwa kucheza na klabu ya Grupo Desportivo Sagrada Esperança ya Angola katika hatua ya 16 bora ambapo mechi zitachezwa nyumbani na ugenini, baada ya hapo timu nane zitaingia katika hatua ya makundi ya michuano hiyo ya Kombe la shirikisho barani Afrika, Grupo Desportivo Sagrada Esperança ilianzishwa December 22 1976 ni klabu changa kwa Yanga iliyoanzishwa 1935.

gfd

Yanga ataanza kucheza nyumbani kati ya Mei 6-8 na mechi za marudiano zitachezwa kati ya Mei 16-18 2016

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

KAMA ULIKOSA VIDEO YA MAGOLI YA MECHI YA KWANZA YANGA VS AL AHLY, FULL TIME 1-1

Soma na hizi

Tupia Comments