Michezo

Arsenal yaifunga Man City katika dimba la Emirates, Mesut Ozil kaendeleza rekodi yake (+Pichaz&Video)

on

Ligi Kuu Uingereza imeendelea usiku wa December 21 kwa mchezo mmoja kupigwa katika dimba la Emirates, Arsenal waliikaribisha Manchester City katika dimba hilo. Huu ndio mchezo uliokuwa unavutia zaidi kuliko mechi zote za Uingereza zilizopigwa weekend ya December 19 na 20.

3290

Mvuto wa mchezo huu unakuja kutokana na timu zote kuwa katika nafasi tatu za juu, hivyo ushindi kwa kila timu ulikuwa ni muhimu kwani utakuwa unamuweka karibu na Leicester City inayoongoza. Hata hivyo kwa takwimu za mechi tano za mwisho kukutana kati ya Arsenal dhidi ya Man City, Arsenal inaonesha kuwa na rekodi nzuri.

3157

Kwani imeshinda mechi mbili kati ya tano dhidi ya Man City, imetoka sare mbili na kufungwa mechi moja. Takwimu zilizidi kuwa rafiki kwa Arsenal baada ya dakika ya 33 Theo Walcott kupachika goli la kwanza kwa Arsenal, huku mambo yakizidi kuwa mabaya kwa Man City. Lakini nyota wa Arsenal Mesut Ozil mfalme wa assist ndio aliotengeneza magoli yote mawili ya Arsenal.

4779

Arsenal kupitia kwa mshambuliaji wake wa kifaransa Oliver Giroud alipachika wavuni goli la pili dakika ya 45 na kuufanya mchezo kumalizika kwa Arsenal kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Man City, huku goli la Man City likifungwa na Yaya Toure dakika ya 82. Kwa matokeo hayo Arsenal wanakuwa nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi wakiwa na jumla ya point 36 tofauti ya point 2 na Leicester City wanaoongoza Ligi.

4238

Video za magoli ya mechi ya Arsenal Vs Man City

https://youtu.be/E0K698c3384

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments