Taarifa zilizoenea mitandaoni usiku wa August 17 ni kuhusiana na jiji la Barcelona ambapo inatokea moja kati ya vilabu bora duniani FC Barcelona, kutokea kwa shambulio linalotajwa kuwa la kigaidi.
Jiji Barcelona limetokea shambulio la kigaidi ambapo dereva wa gari amegonga umati wa watu kwa kukusudia tukio ambalo limepelekea watu 13 kupoteza maisha na zaidi ya 100 kujeruhiwa.
Tukio hilo limetokea katika jiji la Barcelona karibu na Las Ramblas eneo ambao ni maarufu kwa utalii jijini Barcelona, Rais wa Catalan Carles Puigdemont ametangaza kuwa tayari watu wawili wanaoshukiwa kuhusika na tukio hilo wamekamatwa, Polisi wanaendelea kumtafuta dereva wa gari ambaye alitoroka baada ya tukio.