Katibu itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi ‘CCM’, Humphrey Polepole amesema kupitia kipindi cha Mada moto cha Chanel Ten kuwa chama hicho kinampango wakufungua chuo Kikuu cha CCM ambacho kitatoa mafunzo kwa wanachama, makada na viongozi wote wa chama na hata waliopo serikalini kupitia chama ilikuwafundisha itikadi za chama.
“Unajua chama cha Mapinduzi na chama cha kikominist (Uchina) ni marafiki, tumeamua tujenge chuo kikuu cha chama cha mapinduzi ambacho kitakuwa na kazi ya kuwafundisha wanachama, makada,viongozi na wale waliopata dhamana serikalini”-Humphrey Polepole
Aidha Polepole amesema…..>>>Kupitia chama cha mapinduzi tutawafundisha ili tuelewane itikadi yetu, watu hujiunga na chama si kwa ajili ya ushabiki ila watu wanajiunga na chama kwa sababu wanaamini wameielewa itikadi ya chama hiki ni nini”-Humphrey Polepole
ULIKOSA? Kilichosemwa na CCM kuhusu madai ya baa la njaa Tanzania, Bonyeza play hapa chini kutazama