Usiku wa April 22 2017 timu ya Chelsea ya London imefanikiwa kuingia hatua ya fainali ya Kombe la FA England baada ya kuitoa timu ya Tottenham Hotspurs ya London katika mchezo wa nusu fainali ya FA msimu wa 2016/2017, Chelsea na Tottenham wana upinzani mkubwa kutokana na kutoka mji mmoja.
Chelsea wamefanikiwa kuingia fainali ya FA kwa mara ya 14 katika historia baada ya kufanikiwa kuifunga Tottenham kwa jumla ya magoli 4-2, magoli ya Chelsea yakifungwa na Willian dakika ya 5 na dakika ya 43 kwa mkwaju wa penati kabla ya Eden Hazard kufunga goli la tatu dakika ya 75 na Nemanja Matic kuhitimisha ushindi huo kwa kufunga goli la mwisho.
Magoli ya Tottenham yalifungwa na Harry Kane dakika ya 18 na Dele Alli dakika ya 52, hii ni game ya 67 kwa Chelsea kuifunga Tottenham katika mara 158 walizowahi kukutana na wamewahi kutoka sare mara 40 na kufungwa mara 51.
Ushindi huo sasa unaifanya Chelsea inayofundishwa na Antonio Conte kusubiri mshindi wa nusu fainali ya kesho kati ya Man City inayofundishwa na Pep Guardiola na Arsenal inayofundishwa na Arsene Wenger, Chelsea kwa sasa imeshinda kila mechi msimu huu ambayo Willian amefunga goli au akiwa ametoa pasi ya goli hii ni mechi ya 11.
https://youtu.be/UWImaSneUmU
VIDEO: Msimamo wa Simba uliyotolewa leo kuhusu point 3 vs Kagera Sugar