Michezo

Hadi June 2011, hii ndio ilikuwa list ya wanasoka wenye uwezo wa kupiga mashuti duniani (+Video)

on

Imekuwa ni kawaida kukumbushana vitu mbalimbali vinayohusu soka mtu wangu wa nguvu na leo December 22, nimeona sio vibaya nikikusogezea list ya mastaa wa soka waliotamba na ambao bado wanatamba kwa kupiga mashuti makali golini mwa timu pinzani. Hii ndio list ya mastaa watano wa soka wanaongoza kwa kupiga mashuti golini.

Roberto Carlos hakuna ambaye hamfahamu huyu jamaa, na kama wapo ni wachache sana, amezaliwa Brazil na  amezitumikia timu mbalimbali ikiwemo Palmeiras na Real Madrid ya Hispania. Anajulikana zaidi kwa ufundi wa kupiga faulo, anakumbukwa zaidi kwa faulo aliyoipiga na kutikisa nyavu dhidi ya Ufaransa mwaka 1997.

Frank Lampard amezaliwa na kukulia Uingereza, anatajwa kuwa miongoni mwa viungo bora zaidi kuwahi kutokea Uingereza. Lampard ni mzuri katika upigaji wa faulo, kwa sasa anaitumikia New York City ya Marekani.

Cristiano Ronaldo hakuna asiyemfahamu huyu jamaa, kwa sasa anaichezea Real Madrid ya HispaniaRonaldo amekuwa na umahiri zaidi kwa kupiga mashuti kwa kutumia miguu yote miwili anapokuwa uwanjani. Ni mshindi wa tuzo za tatu za Ballon d’Or , amewahi kuichezea klabu ya Manchester United ya Uingereza.

Michael Essien ni mchezaji wa kimataifa wa Ghana ambaye amewahi kuichezea klabu ya Chelsea, ni kiungo ambaye yupo kwenye hii list ya wapiga mashuti makali kuwahi kutokea. Essien kwa sasa anaichezea klabu ya Panathinaikos inayoshiriki Ligi Kuu Ugiriki.

Andrea Pirlo ni kiungo kutoka Italia na amewahi kuvitumikia vilabu tofauti tofauti vikubwa barani Ulaya ikiwemo Inter Millan na AC Millan na kupata mafanikio makubwa ikiwemo kutwaa mataji ya UEFA na Ligi, Pirlo amewahi kutwaa Kombe la Dunia akiwa na timu yake ya taifa Italia mwaka 2006 Ujerumani. Pirlo ni fundi anayetajwa kuwa bora muda wote katika upigaji wa faulo pamoja na mashuti makali nje ya 18. Pirlo kwa sasa anaichezea klabu ya New York City ambayo Frank Lampard anaitumikia pia.

STORI KUTOKA: bleacherreport.com

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments