Michezo

Kuelekea dirisha dogo la usajili barani Ulaya, huu ni usajili mbovu wa wachezaji uliowahi kufanyika …

on

Mtu wangu wa nguvu najua headlines za usajili wa dirisha dogo kwa Bongo zimepita na sasa tunaelekea katika usajili wa dirisha dogo la mwezi January barani Ulaya, tumeona vilabu vya Man United na Tottenham Hotspurs vikiwania saini ya mchezaji wa Algeria anayekipiga katika klabu ya Leicester City Riyad Mahrez. Mtu wangu wa nguvu kabla ya dirisha la usajili la mwezi January halijafunguliwa naomba nikuletee usajili mbovu kuwahi kufanyika katika soka.

5- Chriss Samba zilitumika pound milioni 12.5 kumtoa klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi na kumleta Uingereza katika klabu ya Queens Park Rangers (QPR). Licha kupewa imani ya kufanya vizuri ndani ya klabu hiyo, Samba hakufanya vizuri na mwaka mmoja baada ya kujiunga na QPR alirudi Anzhi Makhachkala.

Samba_1664718a

Chriss Samba

4- Zlatan Ibrahimovic huu ni uhamisho ambao ulifanyika mwaka 2009 wa Zlatan kutoka Inter Milan kwenda FC Barcelona kwa dau la pound milioni 42.5 sambamba na FC Barcelona kumtoa Samuel Eto’o kwenda Inter Milan kama sehemu ya makubaliano yao ili wampate Zlatan Ibrahimovic. Licha ya kusajiliwa kwa dau kubwa Zlatan alishindwa kufanya vizuri sana na Barcelona, Kwani FC Barcelona waliamua kumuuza kwa dau la pound milioni 20.5 kwenda AC Milan ya Italia.

hi-res-90209024_crop_north

Zlatan Ibrahimovic

3- Fernando Morientes huyu ni nyota ambaye alisajiliwa kwa dau la pound milioni 6.3 kutoka Real Madrid kwenda Liverpool mwaka 2005, lakini aliuzwa mwaka 2006 baada ya kucheza jumla ya mechi 41 na kufunga goli 8 pekee, rekodi ambayo sio rafiki kwa mshambuliaji kuwa na takwimu hizo.

51963113

Fernando Morientes wa kushoto akiwa na kocha wa zamani wa klabu ya Liverpool Rafael Benitez

2- Andy Carroll huyu ni staa ambaye alitamba katika klabu ya Newcastle United, hivyo mwaka 2011 baada ya Torres kutimkia Chelsea, Liverpool walitoa dau la pound milioni 35 ili kumsajili nyota huyo kama mbadala wa Torres. Lakini alishindwa kufanya vizuri na mwaka 2013 alitolewa kwa mkopo kwenda West Ham United, huku akiwa kacheza jumla ya mechi 44 na kufunga magoli 6 akiwa na Liverpool.

Andy Carroll of Liverpool looks dejected during the Barclays Premier League match between Manchester City and Liverpool at the Etihad Stadium

Andy Carroll

1- Fernando Torres huu ndio unatajwa kuwa usajili mbovu uliowahi kufanyika mwezi January. Usajili wa Torres kutoka Liverpool kwenda Chelsea mwaka 2011 uliigharimu Chelsea pound milioni 50. Huu ulikuwa ni moja kati ya usajili wa ada kubwa katika usajili wa vilabu vya Uingereza, unaitwa ni moja kati ya usajili mbovu kutokea ni kwa sababu Torres alishindwa kufanya vizuri Chelsea.

hi-res-108818392_crop_north

Torres baada ya kuwasili Chelsea akiwa na Ancelotti kocha wa zamani wa klabu hiyo.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments