Ilikuwa mwezi sasa zimebaki saa kadhaa ulimwengu kuweza kushuhudia fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayozikutanisha timu kutokea Hispania jiji moja, Atletico Madrid dhidi ya Real Madrid fainali ambayo itachezwa Italia katika mji wa Milan uwanja wa San Siro.
Mtu wangu wa nguvu wakati tunasubiria fainali hiyo kati ya Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid, naomba nikusogezee list ya rekodi tano za UEFA Champions League ambazo hazijawahi kuvunjwa.
1- Kwa sasa Zlatan Ibrahimovic ndio mchezaji aliyefunga magoli sita katika michuano hiyo akiwa na vilabu vya Ajax, Juventus, Inter Milan, Barcelona, AC Milan, Paris Saint-Germain.
2- Paolo Maldini ndio mchezaji anayeshikilia rekodi ya kufunga goli la mapema zaidi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, alifanya hivyo mwaka 2005 akiichezea AC Milan katika mchezo dhidi ya Liverpool, alifunga goli sekunde ya 53.
3- Ryan Giggs anashikilia rekodi ya kufunga magoli katika misimu 16 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
4- Ferenc Puskas ndio mchezaji aliyefunga magoli mengi katika mchezo wa fainali, alifunga magoli manne katika mchezo wa fainali mwaka 1960 akiwa na Real Madrid.
5- Mechi ya fainali yenye magoli mengi zaidi ilikuwa ni mechi kati ya Real Madrid dhidi ya Frankfurt May 18 1960, ilimalizika kwa Real Madrid kuibuka na ushindi wa goli 7-3, hivyo hiyo ndio ilikuwa fainali pekee iliyofungwa jumla ya mengi.
ALL GOALS: Fainali ya FA CUP May 25 2016 Yanga vs Azam FC, Full Time 3-1
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE