Mix

Fahamu alipo Mcameroon huyu pekee aliyewahi kuichezea Manchester United

on

article-2553508-1B3C46F100000578-504_634x435-1Huyu ndio mwafrika pekee kutoka katika nchi ya Afrika Magharibi ( Cameroon ) ambae amewahi kuvaa jezi ya klabu ya Manchester United.

Eric Djemba Djemba, kiungo mkabaji wa timu ya taifa ya Cameroon ‘The Indomitable Lions’ ambae alipata bahati kubwa ya kusajiliwa na Manchester United mwaka 2003 akitokea Nantes ya Ufaransa kwa ada ya uhamisho ya paundi million 3.

Alisajiliwa na kutajwa kuja kuwa mrithi wa kiungo Roy Keane lakini baada ya muda mfupi tu alishindwa kufikia malengo kutokana na kuendekeza starehe hivyo kazi iliyompeleka Old Trafford ikamshinda.
Eric-Djemba-DjembaMwisho wa siku Mcameroon huyu akauzwa kwenda Aston villa ambapo napo alishindwa kung’ara na kuanza taratibu kupotea katika ulimwengu wa soka la kiwango cha juu lakini baada ya kupotea kwa muda muda mrefu, wiki hii kiungo huyu amepata bahati ya kusajiliwa na timu St. Mirren inayoshiriki kwenye ligi kuu ya Scotland.

Djemba ambae  na umri wa miaka 32, amewahi kuchezea club kama Odense na Burnley baada ya kutoka Aston villa kabla ya kwenda Qatar na kisha Urusi.

Tupia Comments