Michezo

Hadi kufikia mwaka 2012 hii ndio ilikuwa TOP 5 ya wachezaji watano wanaochukiwa zaidi katika soka …

on

Mtu wangu wa nguvu najua unafahamu kuwa soka ndio mchezo unaopendwa na watu wengi duniani au unaweza kuita ndio mchezo maarufu sana duniani. Najua umezoea kusikia headlines za soka kila kukicha kuhusu mastaa wake kufanya hivi au vile na vitu vingine vingi. Ila kama ambavyo tumekuwa tukiona watu maarufu kutoka tasnia mbalimbali wakichukiwa basi nimekutana na hii mtandaoni mtu wangu. TOP 5 ya mastaa wa soka wanaochukiwa.

5. Ashley Cole huyu alikuwa beki wa zamani wa vilabu vya Arsenal, Chelsea pamoja na timu yake ya taifa ya Uingereza. Cole alikuwa akitajwa kama moja kati ya mabeki bora wa kushoto ila uamuzi wake wa kuhama Arsenal na kujiunga na Chelsea pamoja na kumcheat mkewe Cherly Cole vilimpungumzia umaarufu na kufanya achukiwe.

ashley-cole_2456651b

Ashley Cole

4-  Sergio Busquets huyu ni moja kati ya wachezaji wanaounda kikosi cha FC Barcelona ya Hispania ila moja kati ya vitu vinavyomjengea chuki ni mchezo wake wa kudanganya (Diving) marefa na kushawishi wachezaji wa timu pinzani  waoneshwe kadi. Kitu ambacho kimempelekea kuchukiwa na mashabiki wa soka.

164386-barcelona-and-spain-midfielder-sergio-busquets

Sergio Busquets

3- Luis Suarez huyu ndio mchezaji anayependa kudanganya sana katika soka ili tu timu yake ishinde, aliwahi kushika mpira kwa makusudi katika nusu fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2010 katika mchezo kati ya timu yake ya taifa ya Uruguay dhidi ya Ghana kitendo kilichopelekea kuoneshwa kadi nyekundu. Sambmba na kujiangusha na matendo yake ya kung’ata wenzake.

Luis-Suarez_3265873

Luis Suarez

2- Pepe huyu ni beki wa kati wa kimataifa wa Ureno kwa sasa anaichezea klabu ya Real Madrid ya Hispania. Pepe amewahi kufanya matukio kadhaa ya utovu wa nidhamu uwanjani sambamba na kucheza faulo za makusudi. Baadhi ya matukio aliowahi kuyafanya Pepe ni kumkanyaga kwa makusudi mkono wa Lionel Messi.

Pepeenfada

Pepe

1- John Terry ni nahodha wa klabu ya Chelsea lakini kitendo cha kutembea na mke wa rafiki na mchezaji mwenzake Wayne Bridge kimemvunjia heshima na mapenzi kwa mashabiki wa soka, sambamba na tambia yake ya ulevi, pamoja na kutoa lugha ya kibaguzi kwa mdogo wa mchezaji mwenzake wa zamani watimu ya taifa Rio Ferdinand.

STOKE ON TRENT, ENGLAND - DECEMBER 22: John Terry of Chelsea celebrates after the Barclays Premier League match between Stoke City and Chelsea at Britannia Stadium on December 22, 2014 in Stoke on Trent, England. (Photo by Michael Regan/Getty Images)

John Terry

Hii ndio video ya TOP 5 yenyewe mtu wangu

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments