AyoTV

VIDEO: Baba yake Ngassa kazungumzia ushirikina uliowahi kufanyika katika soka

on

Bado AyoTV inaendelea kukusogezea exclusive interview na mkongwe wa soka Tanzania Khalfan Ngassa baba mzazi wa winga wa kimataifa wa Tanzania anayeichezea klabu ya Fanja ya Oman Mrisho Ngassa,Kama  utakuwa unakumbuka vizuri siku mbili kabla ya mechi ya Simba na Yanga tulisikia sijui nazi zimekamatwa uwanja wa taifa vitu ambavyo vinahusishwa na ushirikina.

Mzee Ngassa amekubali kueleza experience yake katika soka katika kipindi wao wanacheza walikuwa wanafanya mambo ya kishirikiana katika soka, wanaamini iliwahi kuwasaidia?

“Hayo mambo yalikuwepo na hadi sasa hivi bado yanaendelea katika soka letu, sisi wakati tunacheza yalikuwepo unakuta mganga anakuja anawapakapaka madawa halafu mnapanda gari anawaambia msiongee na mtu halafu mnafungwa, kwa hiyo hizo imani zipo”

ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1

Soma na hizi

Tupia Comments