Michezo

PICHA 3: Staa wa FC Barcelona anavyoendelea kula raha Serengeti na mpenzi wake

on

Kiungo mpya wa club ya FC Barcelona ya Hispania na timu ya taifa ya Uholanzi Frenkie De Jong imeonekana anafurahia likizo ya maisha yake nchini Tanzania akiwa katika hifadhi ya taifa ya Serengeti ambako kaambatana na mpenzi wake Mikky Kiemeney.

De Jong ameonekana kuvutiwa kuja Tanzania likizo, huo ukiwa ni mfululizo wa mastaa mbalimbali wa soka duniani, ambao wameendelea kumiminika kuja Tanzania kwa ajili ya mapumziko, miongoni mwa mastaa wa soka ambao wamewahi kuja Tanzania ni pamoja na Martin Skirtel aliyekuwa Liverpool, Mousa Sissoko wa Tottenham, Christian Eriksen na David Beckham aliyekuja na familia yake.

Frenkie De Jong kuanzia msimu wa 2019/2020 tutaanza kumuona FC Barcelona baada ya msimu uliopita wa 2018/2019 kuichezea Ajax FC na kuifikisha hatua ya nusu fainali ya michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2018/2019.

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

Soma na hizi

Tupia Comments