AyoTV

VIDEO: Mechi ya Europa League ambayo Samatta aliihofia na kuhisi hahitajiki uwanjani

on

Usiku wa leo November 24 2016 saa 23:05 nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta atakuwa akicheza mchezo wake wa tano wa hatua ya Makundi ya UEFA Europa League akiwa na KRC Genk dhidi ya timu ya Rapid Wien ya Austria.

Samatta tayari amecheza mechi nne za Europa League hatua ya makundi akiwa na KRC Genk, AyoTV kabla ya mchezo wa leo imempata katika exclusive interview na amekubali kueleza ni mechi ipi aliiona ngumu kwake katika mechi nne za Europa League alizocheza hatua ya Makundi.

“Mechi niliyokuwa nahisi ina chalenji kubwa kati ya mechi nne, ilikuwa ni game ya KRC Genk dhidi ya  Sassuolo kutoka Italia, tulikuwa nyumbani lakini jamaa walikuwa wanamiliki mpira kwa kiasi kikubwa, hiyo mechi nilianzia nje kwa sababu nilikuwa natoka majeruhi lakini presha yake ilikuwa kubwa”

VIDEO: Sababu iliyomfanya Samatta aanze kutumia viatu vya Nike na kuviacha vya Adidas

Soma na hizi

Tupia Comments