Mix

Baada ya kumwagia fedha, Mayweather amuonesha McGregor saa ya Tsh. 3bil

on

Baada ya kummwagia fedha walipokuwa New York bado Mayweather hakumuacha salama McGregor walipokutana tena SSE Arena, Wembley, London mara hii akimtambia kwa kumuonesha saa yenye thamani ya dollar 1.4 milioni (£1.06m), ambazo ni zaidi ya Tsh. 3 bilioni.

Hatua hiyo ilikuja baada ya Conor McGregor kumwambia Mayweather kuwa amevaa high heels walipokuwa kwenye ziara London kuelekea pambano lao.

Tunahesabu siku 40 kuanzia leo ili kuifikia August 26 tarehe ambayo inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa mchezo wa ngumi duniani kote kushuhudia pambano kati ya Floyd Mayweather vs Conor McGregor litakalopigwa T Mobile Arena, Las Vegas ambapo Mayweather atavuna paundi 78m sawa na Tsh. 228.3 Bilioni.

Mtanzania aliyewahi kuweka rehani gari lake kumsadia kijana ada ya Shule!!!

Soma na hizi

Tupia Comments