AyoTV

VIDEO:Yusuph Mlela ameomba pambano la ngumi na Nay wa Mitego

By

on

Kumekuwa na mvutano wa maneno mitandaoni baada ya baadhi ya  wasanii wa Bongomovie kuandamana kwa lengo la kutaka wafanyabiashara wanaouza filamu za nje ya nchi wafungiwe kwani hawafuati  taratibu ambazo wasanii wa bongomovie wanazifata wakati wa usambazaji wa kazi zao.

Nay wa Mitego  alitumia ukurasa wake wa Instagram kuelezea namna gani anaona uamuzi waliochukua wasanii hao usivyo na maana na amewataka wafanye kazi bora pia waache kutoa visingizio visivyo na maana kupitia video aliyoweka kwenye Instagram yake.

Baada ya video ile, muigizaji Yusuph Mlela amemuandikia Nay wa Mitego ombi la mpambano wa ngumi baada ya kuona video ile ambayo Nay aliipost na kuponda uamuzi wa wasanii wa Bongomovie kuandamana.

Tazama video hapa chini kuelewa zaidi mkasa mzima>>>

Video: Shamsa Ford aelezea kisa cha yeye kupigwa ngumi usoni >>>

Soma na hizi

Tupia Comments