AyoTV

MIAKA 20 YA ZIFF: Filamu ya kwanza ya Tanzania kufungua Tamasha la ZIFF 2017

on

Tamasha kubwa la Kimataifa la Filamu linalofanyika kila mwaka Visiwani Zanzibar maarufu kama Zanzibar International Film Festival (ZIFF) mwaka huu linafikisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwake ambapo tofauti na miaka iliyopita, litakuwa na vitu vingi vya ziada vikiwemo viwili vikubwa.

Miongoni mwa mambo yanayotarajiwa kushuhudiwa kwenye Tamasha la mwaka huu ni pamoja na nyongeza za tuzo mbalimbali zikiambatana na fedha huku kwa mara ya kwanza Tamasha hilo litafunguliwa na Filamu ya Tanzania na mashindano ya Jahazi kufanyika mara mbili.

Kaimu Mkurugenzi wa ZIFF Daniel Nyalusi alisema:>>>”Mwaka huu katika kutimiza miaka 20 ya ZIFF tuna vitu vikubwa viwili tuevianzisha ambavyo ni vipya. Soko Filamu ambalo ni Soko Maalumu kwa ajili ya Filamu na TV content na cha pili kikubwa ni Film Schools. Tunaamini kuwa Film School ni foundation ya Film Industry.

“Kwa hiyo, kwa kuwawezesha na kuwatrain na kuwapa nafasi Wanafunzi ambao wapo katika Vyuo vinavyofundisha Filamu kukutana na watu ambao wapo katika tasnia yao itawapa wao urahisi zaidi na nafasi nzuri ya wao kuingia kwenye industry moja kwa moja.” – Daniel Nyalusi.

Agizo la Serikali kwa Wakuu wa Wilaya kuhusu watupa taka ovyo!!!!

Soma na hizi

Tupia Comments