Michezo

Samatta kaifungia KRC Genk goli mbili vs Club Brugge katika ushindi wa 2-1 (+Video)

on

Usiku wa March 4 2017  nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta aliingia katika uwanja wao wa nyumbani wa Luminus Arena kuitumikia club yake ya KRC Genk katika mchezo wa Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya vinara wa Ligi hiyo Club Brugge.

Katika mchezo huo KRC Genk ambao walikuwa nyumbani walifanikiwa kupata ushindi wa goli 2-1, magoli ya KRC Genk yakifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 5 na 42, katika magoli yote aliyofunga Samatta alipewa pasi na Malinovsky na Alejandro Pozuelo, huku goli la Brugge likifungwa na Izquierdo dakika ya 43.

Matokeo hayo yanaifanya KRC Genk kuendelea kuwa nafasi ya nane katika msimamo wa Ligi Kuu Ubelgiji wakiwa na point 45, wakati Club Brugge wao wakiendelea kuongoza Ligi hiyo inayoshirikisha timu 16 kwa kuwa na jumla ya point 58 sawa na Anderlecht waliyo nafasi ya pili.

ALL GOALS: SIMBA VS MBEYA CITY MARCH 4 2017, FULL TIME 2-2

Soma na hizi

Tupia Comments