Mix

Gazeti la Tanzania lililopewa saa 24 kumuomba radhi Rais Magufuli

on

Onyo limetoka kwenye Idara ya habari maelezo kupitia kwa Mkurugenzi wake Dr. Hassan Abbasi ambapo gazeti lililoandika kichwa cha habari ‘UFISADI NDANI YA OFISI YA JPM‘ limepewa saa 24 kuomba radhi.

Taarifa ya Idara hiyo imesema ‘licha ya habari hiyo kujenga dhana kuwa Rais John Pombe Magufuli anahusika na kinachoitwa ufisadi, msingi wa taarifa husika ni tatizo la manunuzi shirika la elimu Kibaha.

Kwa kuwa ni jambo lililodhahiri kuwa shirika la elimu Kibaha sio ofisi, Idara wala kitengo ndani ya Ofisi ya Rais, Mwandishi na Mhariri wa habari husika wamedhihirisha malengo ya kumchafua Rais binafsi kwa jamii. 

Serikali inawaagiza Wahariri wa gazeti hilo kujitathmini na kuchukua hatua kwa kutumia kifungu cha 410 cha sheria ya huduma za habari 2016 kinachowapa fursa ya kuomba radhi, kwa kumuomba radhi Rais ndani ya saa 24 kuanzia saa kumi jioni ya January 30 2017.

Iwapo wahusika wataona muhali kufanya hivyo, Serikali itachukua hatua kali kwa mujibu wa sheria na masharti ya usajili wa gazeti husika, Tunaendelea kuwashukuru Wanahabari wanaofuata madili ya taaluma. – Dr. Hassan Abbasi.

ULIPITWA? Tazama hapa chini kuona Wanajeshi Makomando wa Tanzania walivyoonyesha uwezo wao mbele ya Rais Magufuli

Soma na hizi

Tupia Comments