Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: Wapenzi wa jinsia moja kupigwa mawe hadharani Kenya?
Share
Notification Show More
Latest News
PICHA: Matukio ya Mkutano Mkuu wa CAF uliyofanyika Tanzania
August 11, 2022
Ndugu abiria kulipwa Milioni 150, Wakili aibua mapya ‘Watu binafsi waliopost meme wajiandae’
August 11, 2022
Ajali Mbaya!! Watu sita wafariki, Polisi wafunguka, chanzo ‘Dereva alikuwa Mwendokasi, lilipinduka’
August 11, 2022
Hafla ya makabidhiano ya data za utafutaji wa Mafuta na Gesi asilia kwa vitalu Zanzibar
August 11, 2022
Ukumbini: Bwana Harusi aonesha video ya mkewe akiwa faragha na shemeji yake chumbani
August 11, 2022
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Mix > Wapenzi wa jinsia moja kupigwa mawe hadharani Kenya?
MixStori Kubwa

Wapenzi wa jinsia moja kupigwa mawe hadharani Kenya?

August 19, 2014
Share
3 Min Read
SHARE
Screen Shot 2014-08-19 at 8.03.13 AM
Nje ya bunge la Kenya.

Ripota wa TZA nchini Kenya Julius Kipkoech anaripoti kwamba nchi hiyo inarejea kwenye headlines kuhusu maswala ya kubuni sheria za kipekee ambapo sasa bunge la kitaifa linapanga kujadili sheria inayopendekezwa kwamba raia yeyote wa kigeni anayepatikana akishiriki uhusiano wa jinsia moja ahukumiwe kupigwa mawe hadharani hadi kufa na kama ni raia wa Kenya basi ahukumiwe kifungo cha maisha jela.

Mwandishi na mdhamini wa sheria hiyo Edward Onwong’a Nyakeriga anapendekeza kuharamishwa kwa ulawiti na kuhukumiwa jela kwa wanaotenda kosa hilo huku akisisitiza >> ‘upo umuhimu wa kuwalinda watoto na vijana ambao wanalengwa na dhulma ambazo kwa mda mrefu zinaepukwa kutokana na mabadiliko, teknolojia na habari isiyo chujwa na watoto mayatima kukosa mwakilishi pamoja na majaribio ya wanaoshiriki uhusiano wa jinsia moja kuwalea watoto ilihali wanaendeleza uhusiano wao’

Mswada huu wa chama cha Republican Liberty Party unaharamisha uhusiano wowote wa jinsia moja na tayari spika wa Bunge la kitaifa Kenya Justin Muturi ameupokea na kuuwasilisha kwa kamati ya sheria bungeni ambayo inatathmini kisha kutoa ripoti kwa bunge.

Screen Shot 2014-08-19 at 8.06.26 AM
Sio kila mmoja anakubaliana na ndoa za jinsia moja hata katika nchi zilizoendelea ambazo Marais wake wanaunga mkono ndoa hizo

Muswada huo pia unapendekeza kupigwa mawe hadharani hadi kufa kwa mtuhumiwa anayepatikana na kosa la kuwalawiti watoto wadogo au anayefanya kitendo hicho na kumuambukiza mtoto virusi vya ukimwi ambapo tayari wabunge 78 wamekubali kuunga mkono muswada huo kuwa sheria na wengine zaidi wanaendelea kushawishiwa.

Haya yanajiri wakati Bunge la kitaifa la Kenya likibuni kikundi mseto cha wabunge kuhusu maisha ya walio katika uhusiano wa jinsia moja na wameahidi kutoa mwelekeo wa jinsi ya kushughulikia jambo hilo huku muswada huu ukitarajiwa kupata upinzani mkali kutoka kwa wanaotetea haki za binadamu.

Mwandishi wa vitabu maarufu nchini Kenya Binyavanga Wainaina amekua miongoni mwa waliojitokeza hadharani na kukiri kushiriki mapenzi ya jinsia moja na wakati huohuo Mashirika ya kutetea haki za wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja hivi karibuni yaliwasilisha pendekezo la kutaka Wabunge kuondoa sheria zote zinazowazuia kuishi maisha yao kama watu wengine.

Katiba ya Kenya mwaka 2010 imeharamisha ndoa ya jinsia moja japo haiharamishi moja kwa moja uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja ambapo pia mwezi uliopita utafiti uliofanywa na kampuni ya Ipsos Synovate umeonyesha kwamba 64% ya Wakenya wanaamini kwamba hisia za kushiriki mapenzi na jinsia sawa ni jambo la kujifunza ilihali 14% kati yao wanaamini watu hao huzaliwa walivyo.

Baada ya kuisoma hii stori unaweza kuacha maoni yako kwenye comments hapa chini.

You Might Also Like

Mwana FA alivyoungana na Viongozi mbalimbali kuhamasisha Zoezi la Sensa, Masuguru Wilayani Muheza

Bwawa la Mwalimu nyerere sasa kazi ni Usiku na Mchana, ‘kukamilika June 2024’ Waziri Makamba anena

Picha:Kutoka kwenye shangwe za Simba DAY uwanja wa Mkapa Dar es Slaam

Watalii zaidi ya 30 watembelea maporomoko ya Maji Hululu

Kampuni ya PAET imewekeza Dola Milioni 70 uendelezaji gesi

Millard Ayo August 19, 2014
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article ‘Mfalme wa mapenzi’ ya Sanaipei imegonga views zaidi ya laki 3.
Next Article Alichoandika Maulid Kitenge baada ya kuacha kazi ITV/RadioOne
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

PICHA: Matukio ya Mkutano Mkuu wa CAF uliyofanyika Tanzania
Sports August 11, 2022
Ndugu abiria kulipwa Milioni 150, Wakili aibua mapya ‘Watu binafsi waliopost meme wajiandae’
Top Stories August 11, 2022
Ajali Mbaya!! Watu sita wafariki, Polisi wafunguka, chanzo ‘Dereva alikuwa Mwendokasi, lilipinduka’
Top Stories August 11, 2022
Hafla ya makabidhiano ya data za utafutaji wa Mafuta na Gesi asilia kwa vitalu Zanzibar
Top Stories August 11, 2022

You Might also Like

Top Stories

Ndugu abiria kulipwa Milioni 150, Wakili aibua mapya ‘Watu binafsi waliopost meme wajiandae’

August 11, 2022
Top Stories

Ajali Mbaya!! Watu sita wafariki, Polisi wafunguka, chanzo ‘Dereva alikuwa Mwendokasi, lilipinduka’

August 11, 2022
Top Stories

Ukumbini: Bwana Harusi aonesha video ya mkewe akiwa faragha na shemeji yake chumbani

August 11, 2022
Top Stories

“Marufuku kuingia na silaha Taifa” Kamanda Muliro

August 11, 2022
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?