Habari za Mastaa

Unajua mauzo ya album ya Noorah ilikuaje? Diamond ana ujumbe kwa wasanii TZ.. Nay kasemaje picha yake na Shamsa?

on

radioWasanii wengi TZ wamekuwa wakilalamikia muziki wa Nigeria kuonekana kuteka muziki wa Bongo Fleva kiasi cha kuwafanya na wao kuwaiga.

diamond-platnumz

Kwenye 255 kasikika Diamond Platnumz, amesema ishu sio wasanii kulalamika.. kinachotakiwa kufanyika ni wasanii wa Bongo kutengeneza nyimbo zitakazokuwa kali kuliko za kwao.. muziki wa TZ umeshakua, kinachotakiwa ni kuzuia soko la nje lisiteke muziki wa bongo kwa kutoa kazi nzuri zaidi.

noorah (1)Noorah nae yuko kwenye HEADLINES tena leo, amesema album aliyowahi kutoa haikuuza nakala nyingi kwa sababu kipindi hicho mtindo wa  kucopy CD ndio ulikuwa unaanza, ilimharibia na kufanya apate hela kidogo sana, watu wengi walikosa mwamko wa kununua CD wakati huo.

Kumbe jamaa aliwahi kukatazwa na baba yake kufanya muziki, ilifika wakati akakubaliana na mtoto wake kufanya muziki japo hakumpa msaada wowote.

DDDDDDDDDDDDDDDDDDEEEEEEEEEMuigizaji Shamsa Ford alikuwa wa kwanza kujibu kuhusu picha aliyopiga na msanii Nay Wa Mitego ikionesha wako mapenzini, akasema hiyo ilikuwa promo ya movie mpya wanayofanya.

Leo kwenye 255  mwanamuziki Nay Wa Mitego amesema Shamsa ni rafiki yake kikazi ingawa watu wanahisi kuwa wako kwenye uhusiano  jambo ambalo sio la kweli.

Nay amesema Shamsa nd’o alikuja na hiyo idea ya movie na kumshirikisha kwenye baadhi ya scene, ikikamilika kila mtu ataona kilichoendelea.

 Ili kusikiliza story zote za 255 ya leo bonyeza play hapa chini…

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>>  Twitter Insta FB  na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments