Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

255 ya leo February 12, inawahusu Flaviana Matata, Miss TZ Lilian Kamazima na msanii T.I.D

on

uzinduzi-waFMF-stationaries-project-za-flavianafoundationa-30-of-133

Flaviana Matata

Sikiliza 255 ya leo February 12 kutoka kwenye show ya XXL ya Clouds FM, story ya kwanza kusikika inamhusu mwanamitindo Flaviana Matata ambapo mratibu wake amezungumzia kampeni iliyokuwa inafanywa na Flaviana Matata Foundation ya kuchangia vifaa vya kujenga Shule ya msingi Msinune iliyoko Bagamoyo, amesema baadhi ya michango imeshakamilika na miezi michache ijayo michango hiyo ikiwemo madawati vitakabidhiwa kwenye Shule hiyo.

11 (1) Baada ya shindano la Miss Tanzania kufungiwa, Miss Tanzania 2014 Liliani Kamazima amesema kuwa atashiriki kama kawaida kwenye Miss World, kuhusu kufungiwa kwa mashindano hayo amesema hatua hiyo imeziba ndoto za wasichana waliotaka kushiriki shindano hilo.

q-chief6Kwenye 255 jana Feb 11 Q Chillah alisikika akisema kwamba hayuko tayari kurudi kufanya kazi na TID kwenye Top Band, leo 255 imemtafuta TID ambaye amesema yeye hawezi kujibu chochote kwenye hilo kwa kuwa aliliongelea akijibu swali aliloulizwa na mtangazaji hivyo haikupaswa kuwa story ndefu kufika iliko sasa hivi.

Sikiliza 255 yote hapa kwa kubonyeza play hapa.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments