Habari za Mastaa

255 ya March 6, TID kupiga show, Utaratibu mpya kwenye muziki, bodyguard wa Diamond kwenye mieleka…

on

entertainment_news_stopimageInfo ya kwanza kusikika kwenye 255 ya March 6, ni  ishu ya bodyguard wa msanii Diamond Platnumz anayefahamika kama Mwarabu Suleimani ambaye alikuwa Tajikistan kushiriki kwenye mashindano ya kupigana ya mieleka ambayo yalikuwa na washiriki kutoka mataifa mbalimbali.

LIVINGSTONE MKOI (3) (2)Mwarabu amesema mchezo wa kwanza alicheza na jamaa wa Italy na game ya pili alicheza na jamaa kutoka Iran lakini matokeo hayakuwa mabaya tofauti na alivyotegemea, siku mbili kabla ya pambano la mwisho alipata jeraha mguuni wakati akifanya mazoezi na kupoteza michezo miwili.

tid4Weekend hii msanii TID kwa kushirikiana na Radar Entertainment pamoja na msanii Nazizi kutoka Kenya watafanya show Club Bilz, akizungumza kwenye 255 TID amesema amejipanga vema kwa kuwa ni show yake ya kwanza mwaka huu na kutakuwa na wasanii mabalimbali pamoja na surprise za kutosha pamoja na uzinduzi wa video ya msanii Masai Sharo.

nikiStory ya mwisho kusikika inahusu uzinduzi uliofanyika jana wa program mpya chini ya msimamizi wa hakimiliki wa Afrika Mashariki (East African Copyright Management) ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.

Utaratibu mpya ambao utasimamiwa na program hiyo ni ishu ya wasanii kulipwa na vyombo vya habari vinavyocheza kazi zao, msanii Nikki Wa Pili ni miongoni mwa wasanii waliohudhuria ambaye amesema itasaidia msanii kupata matunda ya kazi anayoifanya.

Ili uweze kusikiliza story zote za kwenye 255 ya leo bonyeza play hapa chini.

Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments