Habari za Mastaa

Ile Pishu ya Kajala inatoka lini?.. Bongo All Star Bash ni nini? Malalamiko ya #KTMA2015, kilichojibiwa je??

on

Microphone

Kesho Ijumaa ya April 01 ndiyo siku ambayo itakuwa inafanyika show  ya ‘Zari All White Party’ pale Mlimani City Dar mtu wangu.. lakini kwa upande mwingine kumbe tutakuwa na burubani kwenye ulimwengu wa Bongo Movie.. YES.. mwigizaji Kajala atazindua movie yake mpya inayoitwa ‘PISHU’.

Kasikika kwenye 255 Kajala, amesema mpango wake ni kuisambaza movie hiyo yeye mwenyewe.. kingine alichokisema ni kwamba hakuna ukweli wowote kwenye story kwamba wasanii wa kike wa Bongo movie ambao wanafanya vizuri wanahongwa na wanaume.

image2Wiki ijayo Dj Stevie B anategemea kufanya show itakayowakutanisha wasanii  mbalimbali ya Bongo Fleva.. akizungumzia show hiyo Stevie B amesema anafanya kitu ambacho kitawakutanisha wasanii wa zamani na wa sasa.

Tamasha linaloitwa Bongo All Star BashBAS BASH pia  watakuwepo mastaa watangazaji wa Radio na Television, wachezaji wa mpira wa miguu, wachekeshaji na wanasiasa.

List ya baadhi ya wasanii watakaoshiriki ni Fid Q, Joh Makini , Mr Blue, Crazy Gk, Izzo Busness, Tid, Belle 9, Mo MusicMkomando na wengine.

IMG_9596

April 29 majina ya wasanii wanaowania Tuzo za KTMA 2015 yalitangazwa ambapo watu mbalimbali wameonekana kulalamikia uteuzi huo kwenye baadhi ya vipengele.

Mratibu mkuu wa Tuzo hizo kutoka BASATA, Gershom Malegesi amesema hawajapata malalamiko ila watu ndio wanapendekeza majina na baadae wana-academy  ndio wanapiga kura ya kumuingiza mshiriki kwa hiyo inawezekana kura zilizopigwa hazikutosha.

Bonyeza play hapa chini kusikiliza story zote…

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter,Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments