Habari za Mastaa

Ben Pol ana Management mpya? Mirabaha inawafikia wasanii TZ? Kingine kipya KTMA 2015… #255

on

headphones-592196_640

Wiki iliyopita Msanii Ben Pol alisign mkataba na management mpya ya  Pan Music ambayo ni ya tatu tangu aingie kwenye muziki.

Image000055Ben Pol amesema mtu aliyekuwa anafanya nae kazi  mwanzo alikuwa anafanya kazi nyingine na kuwafanya wakose muda wa kuandaa show au kutafuta show tofauti, lakini management ya sasa  ambayo ni fulltime na anategemea itafanya kitu kikubwa zaidi kwenye muziki wake kumpeleka kwenye level za kimataifa.

2

Afisa mtendaji mkuu kutoka COSOTA Doreen Anthony amesema wameanza kupokea mirabaha ya wasanii kutoka Kenya.. Doreen amesema TZ nayo inatakiwa kupeleka mirabaha pamoja na vyombo vya habari kulipia na kutoa taarifa ili na wao waweze kupata mirabaha yao.

Doreen amesema msanii aliyepata fedha nyingi kutoka Kenya ni Mwimbaji wa nyimbo za Injili Upendo Nkone na kundi la TMK Wanaume.

Leo majina ya wasanii waliochaguliwa kuingia kwenye Tuzo za KTMA 2014/2015 yametangazwa ambapo mratibu mkuu wa Tuzo hizo kutoka BASATA, Gershom Malegesi ameitaja list nzima.. majina ya mastaa walioongoza kwa kuteuliwa kwenye vipengele vingi zaidi  ni Ali KibaJux na Diamond Platnumz.

Kusikiliza stori zote bonyeza play hapa chini…

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter,Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa>>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments