Habari za Mastaa

Said Fella kuanza biashara ya kuuza album? Eti Black Rhino kaacha kazi, kisa? Iko na story ya DC Makonda.. #255

on

255

millardayo.com ilikusogezea story kwamba Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kaanzisha shindano la kukusaka vipaji vya vijana wanaoimba na kudance katika Wilaya ya Kinondoni.

DSC_02832

DC. Paul Makonda

Leo kasikika kwenye 255 ile time ya XXL, Paul Makonda amesema washiriki wataanza kuchukua form kuanzia wiki ijayo kwa ajili ya usaili wa shindano hilo ambalo litafanyika miezi miwili.

Makonda amesema fainali za mashindano hayo kutakuwa na mabalozi zaidi ya 40, kutoka nchi mbalimbali pamoja na wasanii wakubwa na wafanyabiashara.

.

Black Rhino

Ni muda mrefu hatujasikia kuhusu Black Rhino, kumbe jamaa aliamua kuacha kazi benki moja ya kimataifa na kuamua kujiajiri !!

Rhino amesema baada kuacha kazi alijiingiza kwenye ujasiriamali kwa kufungua kampuni ya Tour & Safaris, kwa kushirikiana na rafiki yake ambayo inakodisha magari kwa ajili ya matumizi mbalimbali na hiyo ndio biashara ambayo alitamani kuifanya muda mrefu.

ktma2012_workshop_fella

Said Fella

Jana kwenye XXL msanii Dully Sykes alisema anatarajia kutoa album mpya lakini amekubaliana na meneja wa Mkubwa na Wanawe, Said Fella kumuuzia master ya album hiyo ambayo itakuwa na nyimbo zake za zamani pamoja na nyimbo chache mpya.

Leo ilikuwa zamu ya Mkubwa Fella kusikika, amesema ameamua kuongea na wasambazaji ili wafanye biashara  ya album kwa sababu kuna watu wananunua nakala ambazo sio halali.. mpango huo utaanza mwezi wa tano.

Mkubwa Fella amesema ataanza na album ya Yamoto Band  alafu zitafuatia na album ya Chege na Temba, Berry Black, THT, Barnaba, Shaa, Diamond Platnumz, Dully Sykes ambapo jumla zitakuwa album kumi.

Kusikiliza story zote bonyeza play hapa chini…

millardayo.com ndio sehemu yako kuzipata story zote mtu wangu, unaweza kuwa karibu zaidi na mimi kwa kujiunga kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments