255 leo inamuhusu Madaam Rita ambaye alikua akipiga Stori na kipindi cha Power Breakfast ambapo aliulizwa kwanini hakujawahi kupatikana mshindi kutokea upande wa Hiphop na kusema akiwa mzuri anapita, wengi wamekua hawajitokezi wakali na si kwamba wao kama waandaaji hawapendi muziki huo.
Naye Kala Jeremiah na Roma Mkatoliki leo wanatarajia kuachia Video ya nyimbo yao ya‘Nchi ya ahadi‘..kwa niaba ya Kala, Roma amesema haoni kama imechelwa kwani walitaka watu waizoee kwanza nyimbo kwa kuwa video ilikua inahitaji watu wengi sana kama 250 na imewachukua siku nzima kushoot katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar.
Sitti Mtemvu kazungumzia maisha yake mara baada ya kuvuliwa taji la Miss Tanzania na kusema maisha yanaendelea vizuri kwa sababu baada ya kuvuliwa taji amepata ujasiri na nguvu ya kujiamini zaidi.,pia imemfanya ajue wapi anaruhusiwa kuongea na wapi anyamaze, pia amekua kiakili na kuweza kufanya mambo makubwa zaidi.
Isikilize hapa…
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.