Habari za Mastaa

Sababu ya FA kuacha kutoa ngoma mpya, Mr Blue na issue ya kublock wenzake ,Nyumba ya Batuli kuteketea moto…#255 (Audio)

on

PRESS

Mwana FA ni miongoni mwa wasanii ambao inasemekana anaweza kurekodi ngoma moja akairudia hata zaidi ya mara nne.. amesema muziki mzuri lazima uchukue muda mwingi, jamaa anasema hapendi kufanya kitu na baadaye kuwaza kurudia, anasema nyimbo ya ‘Mfalme’ alirudia mara nne… Pia kwa sasa hafikirii kutoa ngoma mpya kutokama na masikio ya watu kugeukia zaidi kwenye siasa, anasubiri mambo yatulie kisha atatoa ngoma.

fa

Mwana FA

Stori za mastaa kuwabock watu kwenye mitandao ya kijamii ni jambo la kawaida, kwa upande wa Mr Blue amesema alishafanyiwa hivo na hata yeye ameshawablock washkaji zake kwa kuwa huwa hapendi watu wanaosema uongo hasa kwenye mambo ya siasa, pia mashabiki ambao wamekuwa wakimkatisha tamaa.

bl

Mr. Blue

Jana msanii wa Bongo Movie Batuli alipata ajali ya moto baada ya nyumba yake anayoishi kuteketea chanzo kikidaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme, mwenyewe amesema nyumba aliyokuwa amepanga ilianza kuungua saa1 usiku wakati yeye akiwa ametoka na alipata taarifa saa3 wakati tayari kila kitu kimeungua…kwa sasa polisi wanaendelea na uchunguzi.

 

batuli

Batuli

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments